Ridhiwani awaonya maofisa rasilimali watu awataka waache roho mbaya
Arusha. Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewataka maofisa rasilimali watu na utawala bora kuacha roho mbaya wanapowahudumia wafanyakazi wenzao. Pia, amewaonya kuacha mara moja utaratibu wa kuzuia mishahara ya watumishi kiholela bila kufuata utaratibu wakilenga kuwakomoa. Ridhiwani ameyasema hayo leo Jumamosi Mei 4, 2024 alipokuwa…