NRA kuunda Serikali yenye Wizara 10 ikishinda uchaguzi
Mirerani. Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Almas Kisabya amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais, ataunda Serikali ndogo yenye wizara zisizozidi 10, lengo likiwa kufanikisha utendaji kazi. Kisabya ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni ya urais leo Ijumaa Septemba 12 mwaka 2025 mjini Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Amesema endapo atachaguliwa…