Mabao ya Freddy yamuibua Phiri
SIMBA mnamkumbuka kocha wenu wa zamani Patrick Phiri? Amewatumia salamu akiwaambia kuwa ilibaki kidogo tu presha ya mashabiki iwaondolee mshambuliji mzuri ambaye sasa ameanza kuonyesha mabao yake. Akizungumza na Mwanaspoti, kocha huyo Mzambia ambaye amewahi kuinoa Simba kwa mafanikio alisema kitendo cha timu hiyo kukosa matokeo mazuri na mashabiki kuongeza presha kwa wachezaji ilikuwa mbaya…