KIMBUNGA “HIDAYA” KIMEZIDI KUSOGEA NA KUFIKIA HADHI YA KIMBUNGA KAMILI
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv, MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” kilichopo katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya nchi yetu. Kimbunga “HIDAYA” kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya pwani ya nchi yetu ambapo hadi kufika saa tisa usiku wa tarehe 03 Mei 2024…