Hivi ndivyo neno ‘dollar’ lilivyozaa daladala
Miji bila daladala hainogi, walijua hilo? Na kwa nini kusiwe na daladala wakati ni ngumu kwa kila mwanamjini kumiliki kipando chake? Kwa lugha ya vijana isiyo rasmi, usafiri wa daladala ndio mpango mzima, maana haubagui mtu, ni wewe, miguu na pesa yako, hata kama usafiri wenyewe baadhi ya nyakati unakengeuka misingi ya utu. Tuyaache hayo,…