Konokono wazua balaa mashambani Mbeya
Mbeya. Wakulima Mikoa ya Songwe na Mbeya wamejikuta katika taharuki kufuatia konokono kushambulia na kuharibu mazao yao shambani. Changamoto ya viumbe hao inatajwa kuanza kutokea tangu mwaka jana ambapo athari haikuwa kubwa kulinganisha na mwaka huu ambapo mvua zinaendelea kunyesha. Wakizungumza na Mwananchi leo Januari 18, baadhi ya wananchi waliokumbwa na uharibifu huo wamesema bado…