Samia ateua majaji wanne Mahakama ya Rufani
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Rufani wanne. Pia ameteua wenyeviti wa bodi na kumpangia kituo cha kazi balozi mmoja. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 10, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka walioteuliwa Latifa Alhinai Mansoor anayekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani….