Askofu Shoo: Waliomshambulia Dk Kitima hawaitakii mema nchi
Moshi. Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo amelaani kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Dk Charles Kitima akisema ni tukio baya. “Tukio la kushambuliwa kwa Dk Kitima linashtusha, linasikitisha na linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na Watanzania. Yeyote aliyetenda unyama…