KONA YA FEDHA BINAFSI: ‘Kubet’ ni chanzo cha utajiri lakini siyo wako
Ni mgahawa uliopo jirani na kituo cha mwendokasi cha Gerezani, Kariakoo ambapo watu wanapata chakula na wengine wanakunywa vinywaji. Pembezoni mwa mgahawa kuna lango la kuingia chini ya ghorofa hilo ambako watu wanaingia na kutoka. Maiko, kijana aliyevalia nadhifu anachomoka kutoka katika shimo hilo na kutokeza kwenye mgahawa, anakaa kwenye kiti huku mikono yake ikifunika…