RAIS MWINYI:TUSIPANDISHE BEI ZA BIDHAA ZA VYAKULA WAKATI WA RAMADHANI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuridhishwa na upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula na kuwataka Wafanyabiashara Kutopandisha Bei wakati Ramadhani itakapoanza. Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipotembelea Masoko ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Darajani kuangalia Mwenendo wa Biashara na Upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula kuelekea Mwezi Wa Ramadhani….