Balama: Kama si Yanga ningeacha soka
CHANGAMOTO katika maisha ni vitu vya kawaida, lakini kuna nyingine huwa zinakatisha tamaa na kama mtu ana roho ndogo ni ngumu kutoboa. Hutokea bahati tu, mtu akizungukwa na watu wenye kujali na kutia moyo na kusaidia ushauri wa kisaikolojia kama ilivyomkuta winga wa zamani wa Yanga, Balama Mapinduzi ‘Kipenseli’ anayefichua alivyobakia kidogo tu aache kucheza…