Hukumu mwanamke aliyeuawa na kuchomwa moto Himo, kusomwa Machi 10
Moshi. Wakati upande wa utetezi ukifunga ushahidi wake katika kesi ya mauaji ya Josephine Mngara (30) aliyeuawa na kuteketezwa kwa kuchomwa moto, hukumu ya kesi hiyo inayovuta hisia za wengi, imepangwa kutolewa Machi 10, 2025. Katika utetezi wao, washtakiwa katika kesi hiyo, Erasto Mollel na wa pili, Samweli Mchaki waliokuwa na shahidi mmoja kila mmoja,…