Rais Samia aruhusu wakuu wa taasisi kumshauri bila hofu
Arusha. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya umma nchini kumwambia ukweli hasa pindi anapowataka wawekeze sehemu ambayo wanaona haiwezi kuwa na tija. Amesema kabla ya kufanya hivyo ni muhimu kufanyika tafiti na kujiridhisha kabla ya kuweka fedha. Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatano Agosti 28, 2024 alipokuwa…