Mazungumzo ya kujadili vita vya Gaza kufanyika Saudi Arabia – DW – 26.04.2024
Wanadiplomasia wakuu wa nchi za Kiarabu na Ulaya wanatarajiwa kuanza kuwasili katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, mwishoni mwa wiki hii kushiriki mkutano wa kilele wa kiuchumi pamoja na mikutano kuhusu vita huko Gaza. Mkutano huo maalum wa siku mbili wa Jukwaa la Kiuchumi la Dunia, umepangwa kuanza siku ya Jumapili, na utawajumuisha…