Bunge la Kenya lapokea hoja ya kumuondosha makamu wa rais – DW – 01.10.2024
Muda mfupi kabla saa 9:00, Spika wa Bunge la Taifa, Moses Wetangula, alifungua kikao ili kuupisha mjadala wa kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua. ikao kilijaa pomoni na wabunge walishangilia kwa kupiga miguu chini wakati hoja hiyo ilipowasilishwa. Gachagua analaumiwa kwa kumdhihaki Rais William Ruto, kueneza ukabila, kujilimbikizia mali kwa njia za ufisadi na kutumia vibaya…