Mwalimu mkuu aliyehukumiwa kwa madai ya kumbaka mwanafunzi aachiwa huru
Bukoba. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamkende iliyopo Kijiji cha Nyamkende Wilaya ya Ngara, Enock Mabula, aliyefungwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake, ameachiliwa huru na Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Mwalimu huyo alihukumiwa kifungo hicho kwa kosa la kwanza la kumbaka mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 16…