Mzee wa miaka 75 kortini akidaiwa kumuua mkewe kwa kumchapa fimbo
Geita. Mkazi wa Kijiji cha Kibanga Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Bujukano Lusana (75) amefikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Geita akishtakiwa kwa kosa la kumuua mkewe bila kukusudia kwa kumchapa na fimbo. Katika shauri hilo namba 29166/2024, anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 195(1) na 198 cha Kanuni ya adhabu sura ya 16…