Mawaziri wa Habari na Teknolojia Afrika kujadili utawala wa mtandao
Dar es Salaam. Mawaziri wa Afrika wanaoongoza wizara kwenye masuala ya habari na teknolojia wanatarajiwa kukutana jijini Dar es Salaam, katika kongamano la Jukwaa la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF) wakijadili mambo muhimu yanayohusu sera, matumizi, kanuni na mambo mengine yanayohusisha uchumi wa kidigitali. Kongamano hilo linalotarajiwa kuanza Mei 29 hadi 31, 2025 limetanguliwa na…