Vifo kutokana na mafuriko Mlimba vyafikia 49
Dar es Salaam. Msemaji wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko katika Halmashauri ya Mlimba, mkoani Morogoro imefikia 49. Msemaji wa Serikali ameeleza hayo leo Aprili 20, 2024 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa juu ya hali ya mafuriko nchini na ratiba ya sherehe ya Muungano itakayofanyika Aprili 26, mwaka huu. …