Jeshi Polisi Ruvuma lasitisha mikutano ya Chadema
Songea. Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, limesitisha mikutano yote iliyopangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ukiwamo wa kuhitimisha ziara ya siku sita ya viongozi wakuu wa chama hicho, uliopangwa kufanyika leo. Leo Alhamisi Aprili 10, 2025 Chadema ilipanga kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Matalawe, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha…