Mchakato wa kumng’oa Naibu Rais wa Kenya waanza
Nairobi. Mpango wa kumwondoa Naibu Rais, Rigathi Gachagua kupitia kura ya kutokuwa na imani naye unazidi kushika kasi, huku baadhi ya wabunge wakisema wameambatisha saini zao kuunga mkono hoja hiyo. Naibu Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge la Kitaifa, Owen Baya alithibitisha jana jioni kuwa ukusanyaji wa saini za wabunge unaendelea na kwamba hoja hiyo…