ACT Wazalendo kusajili wanachama milioni 10 ziara mikoa 22
Dar es Salaam. Chama cha ACT Wazalendo kimejipanga kufanya mambo matatu katika ziara yake ya mikoa 22 Tanzania Bara ikiwemo kuhamasisha wananchi kushiriki kupiga kura na kuzilinda katika vituo vya kupigia kura katika chaguzi zinazokuja. Sambamba na hilo, wamejipanga kusikiliza kero za wananchi na dhumuni lingine ni kusajili wanachama milioni 10 katika ziara hiyo inayotarajiwa…