Kesi ya ‘vigogo wa Kigamboni’ yakwama
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kusikiliza ushahidi katika kesi ya kuchepusha fedha na kuisababishia Wizara ya Tamisemi hasara ya Sh165 milioni, inayowakabili washtakiwa 13, wakiwemo wakuu wa Idara wa Manispaa ya Kigamboni, kutokana na washtakiwa wawili kushindwa kuleta Mahakamani wakitokea gereza za Segerea. Kesi hiyo ilipangwa leo Jumanne Januari 13, 2026…