Mbeya City yazidi kujiimarisha yambeba Kelvin Kingu
BAADA ya kumalizana na Ame Ally akitokea Mashujaa, uongozi wa Mbeya City umemuongezea nguvu mkongwe huyo kwa kunasa saini ya beki wa kati, Kelvin Kingu Pemba kutoka Tabora United kwa mkataba wa mwaka mmoja. Msimu uliopita Pemba alikuwa na kiwango bora sana akiwa na nyuki wa Tabora, lakini klabu hiyo imeshindwa kumbakisha akitimkia Mbeya City…