Wafungwa 1,500 watoroka Maputo katika machafuko ya uchaguzi – DW – 25.12.2024
Mkuu wa Polisi Bernardino Rafael amesema jumla ya wafungwa 1,534 walitoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali lililoko umbali wa takriban kilomita 15 kutoka mji mkuu Maputo. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, alibainisha kuwa kati ya waliokuwa wakijaribu kutoroka, 33 waliuawa na 15 walijeruhiwa katika makabiliano na walinzi wa gereza. Operesheni ya kuwasaka wahalifu…