Serikali yatwishwa zigo vurugu za bodaboda
Dar es Salaam. Mamlaka za usimamizi wa sheria za usalama barabarani zinalalamikiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo, hivyo kuwa chanzo cha vurugu za madereva wa bajaji na bodaboda. Lawama zinaelekezwa kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (Latra) na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani zinazosimamia Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973…