UCHOKOZI WA EDO: Maisha rahisi kwa chawa, magumu kwa Professa
Katika kochi moja refu maeneo ya Kinondoni nilipata bahati na wasaa wa kukaa na kupiga gumzo na mmoja kati ya viongozi waandamizi wa Serikali hii. Waziri mwenye akili zake timamu na mwenye uelewa wa mambo. Aliniuliza kitu ambacho natembea na jibu lake. Bahati nzuri tulikubaliana. Aliniuliza kama kuna ‘afya’ yoyote kwa nchi kwa hiki kinachoendelea…