Mwili waopolewa mtaroni Jangwani | Mwananchi
Dar es Salaam. Mwili wa mtu mmoja umeonekana asubuhi ukielea majini kwenye mtaro uliopo Jangwani, jirani na kilipokuwa kituo cha mabasi ya mwendokasi. Katika eneo hilo kwa sasa unaendelea ujenzi wa barabara mbadala kabla ya kubomolewa ya awali kupisha ujenzi wa daraja la juu litakalounganishwa eneo la Fire na Magomeni. Mwili huo wa mtu mzima…