Uchumi duni watajwa chanzo ongezeko magonjwa sugu kwa jamii
Mbeya. Imebainika kuwa ukosefu wa kipato kwa baadhi ya wananchi ni chanzo cha ongezeko la magonjwa sugu yasiyoambukizwa, kutokana na kukosa fedha kugharamia matibabu na kuzifikia huduma kwa wakati. Hatua hiyo imetajwa kusababisha baadhi ya wananchi wanaobainika na matatizo ya figo, ini, saratani, afya ya akili kufanyiwa uchunguzi wa maradhi hayo tatizo likiwa limeshakuwa sugu….