Pacha wa kike waliojijengea umaarufu kwa kazi ya upagazi Mlima Kilimanjaro
Moshi. Pacha Enjolight na Heavenlight Mafuwe (33), wakazi wa Kijiji cha Uduru, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, wameondoa dhana kwamba kazi ngumu, hususan zinazohitaji msuli na ustahimilivu ni za wanaume pekee. Kazi yao ya upagazi katika Mlima Kilimanjaro imeonyesha wazi kuwa uthubutu, bidii na uthabiti huchaguliwa bila kujali jinsia. Mafanikio yao ni matokeo ya juhudi…