Mzozo Mashariki ya Kati kuathiri bei ya mafuta duniani
Mashambulizi yanayoendelea Mashariki ya Kati yanahofiwa kupandisha bei ya mafuta duniani kutokana na mataifa katika ukanda huo kuwa wazalishaji wakubwa wa mafuta, jambo litakalochochea kupungua kwa mafuta katika soko la dunia. Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran jana Jumamosi, Februari 28, 2026, zikiwalenga viongozi wake na kuitumbukiza Mashariki ya Kati katika mzozo mpya…