Mawakala wapaisha tiketi safari za mikoani
Dar es Salaam. Licha ya mabasi kuwapo, upatikanaji wa tiketi umekuwa na changamoto katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli, jijini Dar es Salaam, mawakala wakizihodhi na kuuza kwa bei ya juu. Kutokana na changamoto hiyo inayosababisha baadhi ya abiria kukata tamaa, wamejikuta wakilazimika kukubaliana na mawakala wa mabasi wanaolangua tiketi. Amina Juma, mfanyabiashara aliyekuwa akielekea…