Yanga yakwama tena kwa Mtibwa, kicheko kwa Simba
Nuksi ya sare imeendelea kuiandama Yanga baada ya jana kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Huo umekuwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Yanga kupata matokeo ya sare tasa katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Azam FC na TRA Unted. Sare hiyo inaonekana kuwa na faida kwa Simba…