
Mawaziri wa EAC wapo Zanzibar kutatua migogoro ya kikanda – DW – 08.07.2024
Mawaziri wa mambo ya nje na wasaidizi wao kutoka nchi nane zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanakutana Zanzibar wakati huu wa changamoto nyingi za kisiasa, kijamii na kiuchumi duniani na kwenye kanda hiyo. Mkutano huo unafanyika wakati Kenya moja ya nchi wanachama imeshuhudia wimbi kubwa la maandamano ya vijana dhidi ya serikali. Naibu Waziri Mkuu na waziri…