
Taka za plastiki zaipasua kichwa Serikali
Arusha. Katika kukabiliana na madhara yatokanayo na kuzagaa kwa taka za plastiki nchini, serikali imewaita wadau wa sekta binafsi kushirikiana kupunguza tatizo hilo ikiwemo kufanya bunifu mbalimbali zenye kuzirejesha katika matumizi. Tanzania inakadiriwa kuzalisha zaidi ya tani milion 20 za taka ngumu kila mwaka, ikiwa ni wastani wa kilo 300 kwa mtu mmoja kwa mwaka…