Kilichojiri kesi ya wanaodaiwa kumuua mwanafamilia
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Februari 26, 2025, kuwasomea hoja za awali (PH) Sophia Mwenda (64) na mwanaye, Alphonce Magombola(36) wanaokabiliwa na kesi ya mauaji. Mwenda ambaye ni mkazi wa Mbagala anadaiwa kushirikiana na mtoto wake huyo wa kiume, kumuua Beatrice Magombola, ambaye ni binti yake wa kumzaa mwenyewe. Uamuzi huo…