RC Chongolo aiwakia halmashauri kwa kutowalipa wazabuni
Songwe. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo ameiagiza halmashauri ya mji wa Tunduma kuwalipa wazabuni madai yao, yanayodaiwa kufika Sh1.8 bilioni tangu mwaka 2019, hali inayosababisha malalamiko mengi. Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya Mkoa (RCC) kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26, Chongolo ameonyesha masikitiko yake…