Siku 170 za Mbowe nje ya siasa
Dar es Salaam. Zimetimia siku 170, tangu Freeman Mbowe alipowekwa kando kwenye uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Tundu Lissu huku maswali yakitawala likiwemo anakwenda wapi? Mbowe aliyeiongoza Chadema kwa miaka 21 kwa nafasi ya uenyekiti, uongozi wake ulitamatika asubuhi ya Januari 22, 2025 baada ya wajumbe…