Mtanzania avumbua jukwaa kuifanya Tanzania kitovu cha usafirishaji kikanda
Katika zama ambazo dunia inakimbilia kidijitali, Tanzania nayo imeanza safari ya kujenga mifumo bunifu inayoweza kuifanya kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji wa mizigo katika Afrika Mashariki. Kupitia CargoLink, jukwaa la kisasa la usafirishaji wa mizigo lililobuniwa na kijana Mtanzania, Azizi Omary Chamani, sekta hiyo (logistics) inatarajia kupata msukumo mpya wa kuongeza ufanisi zaidi, uwazi…