Iran na washirika wajadili kisasi cha mauaji ya Haniyeh – DW – 01.08.2024
Vyanzo vitano tafauti vililiambia shirika la habari la Reuters kuwa mkutano huo wa siku wa Alkhamis (Agosti 1) mjini Tehran ulitazamiwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa makundi ya Islamic Jihad na Hamas kutokea Palestina, Houthi kutoka Yemen, Hizbullah kutoka Lebanon na makundi ya wanamgambo kutoka Iraq. “Iran na wajumbe wa Mshikamano wa Mapambano watakuwa na kikao cha…