Machumu, Tido waula, Nyalandu arudi kivingine

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, amewateua waliowahi kuwa Wakurugenzi watendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Bakari Machumu na Tido Mhando kwenye ofisi yake ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. Uteuzi huo uliofanyika leo Jumatano, Novemba 19, 2025, umemtaja Bakari Machumu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, akichukua nafasi ya Sharifa Nyanga ambaye…

Read More

Polisi aliyeua kwa AK-47 afungwa kifungo cha nje

Tarime. Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Musoma imemhukumu kifungo cha nje cha miezi 12 aliyekuwa Konstebo wa Polisi, Kululutela Nyakai kwa kumuua kwa risasi Ng’ondi Masiaga, aliyetuhumiwa kufanya biashara ya magendo. Masiaga aliuawa kwa kupigwa risasi na bunduki ya kivita AK-47 Machi 31, 2023 katika kijiji cha Kubiterere wilayani Tarime wakati Nyakai na mwenzake…

Read More

Sekta ya madini kuvuka lengo, wadau wachambua

Dodoma/Dar es Salaam. Sekta ya madini nchini imevuka malengo yake baada ya kuchangia asilimia 10.1 ya Pato la Taifa (GDP) mwaka 2024 ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya muda ulilengwa na Serikali kwenye Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano wa sasa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili…

Read More

Nape aeleza Serikali inavyoshughulikia uhalifu mitandaoni 

Dodoma. Serikali imesema uhalifu mtandaoni umeendelea kupungua kutokana na hatua zinazochukuliwa kukabiliana nao. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hayo bungeni leo Mei 15, 2024 akijibu swali la Mbunge wa Buhigwe, Kavejuru Felix. Mbunge huyo amehoji Serikali ina mikakati gani ya kukomesha wizi wa mtandaoni. Akijibu swali hilo, Nape amesema…

Read More

Kimbunga Hidaya sio kitisho tena kwa Tanzania. – DW – 05.05.2024

Serikali ya Tanzania imesema kimbunga hidaya kilichopiga katika pwani ya Afrika Mashariki kimeshapoteza nguvu na sio kitisho tena kwa nchi hiyo. Hata hivyo maafisa wameutaka umma kuendelea kuwa na tahadhari kwasababu kimbunga hicho kimesababisha mvua kubwa na upepo mkali,hali itakayoendelea siku nzima ya Jumapili.  Maeneo mengi ya Tanzania Jumamosi yalikosa umeme huku mvua kubwa ikinyesha…

Read More

Hamdi agawa dakika 270 | Mwanaspoti

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi, ameonekana kuridhishwa na safu yake ya ulinzi huku akizigawa dakika 270 zilizoleta matumaini makubwa. Hamdi ambaye ameiongoza Yanga katika mechi sita za Ligi Kuu Bara, ana jukumu kubwa la kuhakikisha timu hiyo inatetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara iliouchukua misimu mitatu mfululizo. Katika mechi tatu za kwanza ambazo ni…

Read More

Mwamba uliokwamisha ujenzi bandari ya Bukoba wapasuliwa

Bukoba. Upanuzi wa bandari ya Bukoba uliokuwa umesimama kutokana na kukumbwa na changamoto ya mwamba uliobainika chini ya maji katika ziwa Victoria mkoani Kagera, sasa upo katika hali nzuri kufuatia mwamba huo kupasuliwa. Julai 16, 2024 mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Mnanka Maginga akitoa taarifa, aliwaeleza wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Uhamasishaji Biashara waliokuwa…

Read More

Kocha Abdul Saleh amrithi Mngazija Uhamiaji FC

KIKOSI cha Uhamiaji FC kimemtambulisha Abdul Saleh Mohammed kuwa kocha mkuu wa timu hiyo akichukua nafasi ya Ali Bakar Mngazija. Mngazija ambaye ametimkia Coastal Union ya Tanga, aliitumikia Uhamiaji FC kwa msimu mmoja pekee wa 2024-2025 ambapo timu hito ilimaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Zanzibar. Mbali na kufanya maboresho ya benchi la…

Read More