Dar-si-Salama ilivyomfyatua Fyatu na yeye akafyatuka!
Baada ya kukaa majuu kwa ngwe nyingi, kfyatufyatu si nikajitia kiherehere na mbambamba kwenda kujinoma Dar––si––Salama. Badaa ya kwenda Arusha, Moshi, na Ushoto na kufaidi kila kitu na makandokando, likaja wazo la kufyatua kitu hiki na namna nilivyofyatuliwa kulhali. Bila hili wala lile, niliamua kutua Dar-si-Salama japo kujikumbusha zama zangu Dar. Mara hii, sikufikia Kariakoo…