
DKT.NCHIMBI ATUA RASMI SONGEA KUSAKA KURA ZA CCM
Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi amewasili Songea, mkoani Ruvuma leo Septemba 19, 2025. Dk Nchimbi ataungana tena na Mgombea urais wa chama hicho, Dkt.Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwasili kesho ambapo watakutana mkoa mmoja tangu Agosti 28, mwaka huu walipozindua kampeni za chama hicho…