TASAC YATOA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA DODOMA
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC, leo tarehe 02 Juni, 2025 limetoa elimu ya utunzaji wa mazingira majini kwa wadau waliotembelea banda lao jijini Dodoma. TASAC imetoa elimu hiyo kwa wadau na wananchi wa Dodoma katika Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2025 yanayofanyika kuanzia tarehe 01 – 05 Juni, 2025 jijini humo. …