Ripoti Hamdi yashusha wanne Yanga
MIKAKATI ya kukiimarisha kikosi cha Yanga kwa ajili ya msimu ujao, imeanza mapema kwa kocha wa timu hiyo, Hamdi Miloud kuwasilisha ripoti ya usajili ambayo ameainisha nyota wanne anaowataka. Yanga ambayo Jumatatu hii itakuwa Manyara kucheza na Fountain Gate mechi ya Ligi Kuu Bara, inapambana kubeba ubingwa wa michuano hiyo kwa msimu wa nne mfululizo….