
Nyalusi aacha simanzi, viongozi Chadema, wananchi wamlilia
Iringa. Kifo cha Frank Nyalusi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa Jimbo la Iringa Mjini, kimeacha simanzi miongoni mwa wanachama wa chama hicho, viongozi wa kisiasa na wakazi wa Mkoa wa Iringa kwa ujumla. Nyalusi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Septemba 19, 2025, akiwa hospitalini kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji…