Prisons yagoma kushuka, yaichongea Fountain Gate
MAAFANDE wa Tanzania Prisons wamegoma kushuka daraja kwa mara nyingine baada ya kuifumua Fountain Gate mabao 3-1 katika mechi ya marudiano ya play-off iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya. Msimu wa 2021-2022 Prisons ilinusurika pia kushuka daraja kupitia play-off dhidi ya JKT Tanzania kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1, baada ya kushinda ugenini…