Mtandao wa wizi wa pikipiki wafichuliwa, tisa wadakwa Iringa

Iringa. Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limekamata pikipiki 115 na watuhumiwa tisa katika operesheni maalumu iliyovunja mtandao wa wizi na usambazaji wa pikipiki nchini. Akizungumza jana Machi 25, 2026 katika Kituo Kikuu cha Polisi Iringa, Kamanda wa Polisi Mkoa huo,  Allan Bukumbi, alisema operesheni hiyo ilianza Januari 17, 2026 Kihesa, ikihusisha ufuatiliaji wa kina…

Read More

Dkt. Mwigulu: Tuendelee Kumuombea William Lukuvi na Kuifariji Familia Yake

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaomba Watanzania waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, marehemu William Lukuvi aliyefariki jana Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma. Akiongea kwa niaba ya Serikali nyumbani kwa marehemu Area D, jijini Dodoma leo, Alhamisi, Machi…

Read More

Maofisa Polisi 12 mbaroni kwa tuhuma za rushwa Afrika Kusini

Pretoria. Mamlaka kupambana na rushwa nchini Afrika Kusini imewakamata maofisa 12 waandamizi wa polisi kwa tuhuma za rushwa na udanganyifu. Maofisa hao walifikishwa mahakamani jana Jumatano Machi 25, 2026 katika mji mkuu, Pretoria. Miongoni mwa watuhumiwa hao yupo, Kamishna wa Kitaifa wa Polisi, Fannie Masemola ambaye amekabidhiwa hati ya kumtaka afike mahakamani mwezi ujao kuhusiana…

Read More

Tanzania, Djibout kushirikiana biashara ya kaboni

Dodoma. Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) cha Tanzania na Djibouti kupitia tasisi inayoratibu masuala ya Kaboni ya nchi hiyo ya Africa Sovereign Carbon Registry (ASCR) Foundation, zimeanza mazungumzo ya ushirikiano wa kimkakati wa biashara ya kaboni inayohusiana na sekta za usafiri wa anga na majini. Ushirikiano huo unalenga kuhakikisha sekta zinazochafua zaidi mazingira,…

Read More

Lukuvi umeitwa marehemu, oh! Mnyalukolo, Vahungilage…

Dodoma. Gwiji wa muziki Ramadhan Mtoro Ongala (Dk Remmy) aliwahi kuimba wimbo wake kuwa ‘kifo hakina huruma.’ Katika moja ya vitabu vitakatifu kimeandika, kilio kilisikika Rama, Rahel akiwalilia watoto wake asikubali kufarijiwa kwa kuwa hawapo tena na ndivyo ilivyo, kilio kimesikika Dodoma, Rais akimlilia waziri wake kwa kuwa hayupo. Kwenye wimbo huo ametaja mambo kadhaa…

Read More

Mateso na Unyanyasaji wa Kimwili kwa Watoto huko Gaza Yalitangaza Uhalifu wa Kivita – Masuala ya Ulimwenguni

Zaidi ya ukiukwaji mkubwa 8,554 dhidi ya watoto umetokea nchini Israel na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu wakati wa mzozo unaoendelea. Credit: UN News na Thalif Deen (umoja wa mataifa) Alhamisi, Machi 26, 2026 Inter Press Service UMOJA WA MATAIFA, Machi 26 (IPS) – Mgogoro unaoendelea kati ya Israel na Palestina, ambao ulianza Oktoba…

Read More