MNIKWAMBIE MAMA: Mtuletee wagombea wenye sifa ya ubunifu
Endapo utaona tone la mvua likiangukia sofani, utashikwa na hofu ya kuharibika kwa sofa hilo. Utatupa macho juu kuona panapovuja na kukutana na alama kwenye dari. Utaweka ngazi na kuparamia darini ambako utagundua kigae kilichovunjika. Usipoangalia utajikuta ukirudi chini na kuinamisha kichwa: kadha imekuwa kadha wa kadha! Namna hii ndiyo ambayo matatizo huitumia kumchanganya mwanadamu….