Sakata la Simba linavyoweza kuipa Yanga ubingwa
NDO hivyo bwana! Kitendo cha Simba ‘kugomea’ mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga kabla ya Bodi ya Ligi kubariki kwa kuahirisha bila kuzingatia kanuni za Ligi Kuu, kinaifanya timu hiyo ya Msimbazi kujiweka pabaya dhidi ya jinamizi la kutotwaa ubingwa. Mashabiki wa soka kwa sasa wanasikilizia kujua nini itakuwa hatima ya sakata hilo…